1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Waziri mkuu Siniora ashinikizwa kujiuzulu

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCn1

Mgogoro wa kisiasa nchini Lebanon hauonyeshi ishara za kupunguka,huku waandamanaji wanaoiunga mkono Syria wakiendelea kampeni yao ya kutaka kuipindua serikali inayoungwa mkono na nchi za magharibi.Maelfu ya waandamanaji wa Hezbollah na washirika wao,kwa siku ya pili kwa mfululizo, walibakia katika mahema yao kati kati ya mji mkuu Beirut,karibu na ofisi ya waziri mkuu Fouad Siniora.Wakati huo huo,Siniora kwa mara nyingine tena ameapa kuwa hatongólewa madarakani kwa maandamano ya upinzani.Chama cha Kishia cha Hezbollah,kinataka kuipindua serikali ya Lebanon na kinataka serikali yenye umoja wa kitaifa.