1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT.Maadhimisho ya kifo cha Rafik Hariri kuendelea leo kama ilivyopangwa

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSS

Mipango ya kuadhimisha miaka miwili tangu kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri inatarajiwa kuendelea kama ilivyo pangwa hata baada ya shambulio la bomu dhidi ya basi moja kuwauwa watu watatu na kuwajeruhi watu wengine 20 hapo jana, karibu na mji wa Bikfaya ulio kaskazini mwa Beirut, siku moja kabla maadhimisho hayo ambayo yatafanyika hii leo.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limelaani shambulio hilo.

Viongozi wanaoipinga Syria wameitisha mkutano mkubwa leo hii katika mji wa Beirut.

Rafik Hariri aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon aliuwawa pamoja na watu wengine 20 katika shambulio la bomu tarehe kama ya leo,14.mwezi February mwaka 2005.