1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIT HANOUN: Mashambulio ya Israel yameua wanamgambo wa Hamas

5 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvu

Vikosi vya Kiisraeli vimewauwa wanamgambo 7 wa Hamas na raia 2 katika mashambulio yaliofanywa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.Sasa idadi ya Wapalestina waliouawa katika mashambulio ya Israel ya siku nne kwenye mji wa Beit Hanoun imefikia 44.Mwanajeshi mmoja wa Kiisraeli pia ameuawa.Jeshi la Israel linasema,mji wa Beit Hanoun umelengwa kwa sababu mashambulio mengi ya makombora dhidi ya Israel yanafanywa kutoka mji huo.