1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Belarus kununua gesi bei juu.

28 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCfW

Brussels.

Umoja wa Ulaya umeitaka Russia na Belarus kutatua mzozo wao juu ya bei ya gesi kutoka Russia.

Kamishna wa masuala ya nishati wa umoja wa Ulaya amesema katika taarifa kuwa umoja huo unafuatilia hali hiyo kwa karibu kwasababu inaweza kuathiri usambazaji wa gesi katika mataifa wanachama wa umoja huo.

Kampuni la gesi la Russia limetishia kusitisha kuiuzia gesi Belarus ifikapo Januari mosi iwapo haitakubaliana na bei mpya ya nyongeza.

Gazprom linadai kuwa Belarus inapaswa kulipa zaidi ya mara mbili ya bei ya hivi sasa mwaka ujao na itoe nusu ya hisa zake katika mfumo wa usambazaji wa gesi.