1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Belfast. Viongozi watakiwa kuunda serikali ya umoja baada ya uchaguzi.

10 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKd

Kiongozi wa chama cha Democratic Unionist Ian Paisley amekuwa katika hali ya mbinyo mkali jana ili kuweza kupata makubaliano na mahasimu wakuu chama cha Sinn Fein baada ya makundi yote hayo mawili yenye msimamo mkali kufanya vizuri katika uchaguzi wa bunge katika Ireland ya kaskazini.

Katika muda wa mwisho uliotolewa na serikali za Uingereza na Ireland, chama cha DUP na Sinn Fein ambavyo vilipata nafasi ya kwanza na ya pili katika uchaguzi wa Jumatano vimepewa hadi March 26 kukubaliana kuhusu kugawana madaraka na kuunda serikali.

Iwapo vyama hivyo viwili , ambavyo hadi hivi karibuni havikuweza kufikiria hata kuzungumza kwa pamoja , licha ya kutawala kwa pamoja , vikifanya hivyo, Paisley anaweza kuwa waziri mkuu wa kwanza na Martin McGuinnes wa chama cha Wakatoliki cha Sinn Fein atakuwa naibu wake.

Lakini mwanasiasa mkongwe Paisley anaonekana kuonyesha dalili ndogo ya kukubali kulegeza kamba katika wakati huu kutokana na historia ya kutokubaliana juu ya madai iwapo Sinn fein itaunga mkono polisi wa Ireland ya kaskazini.