1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BELFAST:Mahasimu wa kisiasa wafikia muafaka wa kihistoria Ireland Kaskazini

27 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCF1

Vyama viwili vikuu hasimu vya Protestant na Catholic, huko Ireland ya Kaskazini, hatimaye vimefikia makubaliano ya kihistoria, ya kuunda serikali ya pamoja ambayo itakuwa na mamlaka katika jimbo hilo la Uingereza.

Ian Paisley kiongozi wa chama cha Democrat Unionist na mwenziye Gerry Adams wa Sinn Fein, waliwaambia waandishi wa habari mjini Belfast ya kwamba makubaliano hayo yataanza rasmi utekelezaji wake tarehe 8 mwezi Mei.

Hiyo inafuatia mazungumzo ya kwanza ya ana kwa ana kati ya viongozi hao.Ian Paisley amekuwa akikataa kukutana uso kwa uso na viongozi wa Sinn Fein.