1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bemba arejea tena DRC

Mitima Delachance, DW, Bukavu24 Juni 2019

Bemba amerudi nchini humo kukiwa na malalamiko chungu tele ya kiusalama, kufuatiliwa kwa wabunge wa kitaifa wa upinzani na pia madai ya kuandaliwa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa katika mikoa.

https://p.dw.com/p/3KzOa
DR Kongo Rückkehr Jean-Pierre Bemba
Picha: AFP/A. Huguet

Jean-Pierre Bemba, mwanasiasa mpinzani  katika  jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo aliwasili mjini Kinshasa Jumapili 23.06.2019, nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, kutoka Brussels Ubelgiji. Hii ni mara ya kwanza kurejea nchi humo tangu Agosti 2018.

Kiongozi huyo anarudi nchini humo kukiwa na malalamiko chungu tele ya kiusalama, kufuatiliwa kwa wabunge wa kitaifa wa upinzani na pia madai ya kuandaliwa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa katika mikoa.

Ndege ya Jean-Pierre Bemba ilitua kwenye uwanja wa ndege wa N'djili mjini Kinshasa na kupokelewa na viongozi wa chama chake cha MLC, lakini pia na viongozi wawili wa muungano wa Lamuka ikiwa ni pamoja na Martin Fayulu na Adolphe Muzito.

Bemba amewasili nchini jamhuri ya Congo wakati huu ambapo asasi za kiraia zikiwa zinapaza sauti kuitaka tume ya uchaguzi iendelee kutekeleza kalenda ya uchaguzi. Baada ya uchaguzi wa Desemba mwaka jana, kalenda hii inapanga pia uchagazi wa serikali za mitaa. Ila hadi hivi sasa, hakuna kinachofanyika kwa kuutayarisha.

Kiongozi wa upinzani DRC Pierre Bemba akiwa katika uwanja wa ndege baada ya kurejea nchini mwake 23.06.2019.
Kiongozi wa upinzani DRC Pierre Bemba akiwa katika uwanja wa ndege baada ya kurejea nchini mwake 23.06.2019.Picha: AFP/A. Huguet

Kalenda ya uchaguzi inapanga kuwa tume ya uchaguzi ingepaswa kuwaandikisha wapiga kura kwa ajili  ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa, ila haikufanya hivyo. Tume ya uchaguzi inazidi pia kulaumu hali yakuwa ni kana kwamba ime sahauliwa sababu tangu mwanzo wa mwaka huu, hakuna pesa kwa ajili ya uchaguzi  huo ilizo zipata kwa kufanya kazi zake. Gaudens Maheshe ambaye ni kiongozi wa tume ya uchaguzi katika mkoa wa Kivu kusini amesema: "Uchaguzi wa kimitaa unagharimu pesa nyingi sana na ndio kwa maana unastahili kutayarishwa vilivyo. Nikweli tungepaswa kuandaa wapiga kura tangu march ishirini na tatu ila hatuku weza. Ingetokana na sisi, kweli tunge andaa uchaguzi huo katika muda unao takika."

Hadi hapo, wakaazi wanazidi kujiuliza uchaguzi huo utafanyika lini sababu tangu tarehe kumi na tatu juni, kuna wanajumbe wa tume ya uchaguzi walioanza kujiuzulu kutokana na kumalizika kwa muhla wao.

Uchaguzi huo wa kimitaa umepangwa tangu uchaguzi wa mwaka 2006i, bado kufanyika.