1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benedict 16 awataka watu kuwa na muda kwa ajili ya Mungu.

25 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfzd

Vatican. Kiongozi wa kanisa Katoliki Pope Benedict wa 16 ameadhimisha siku kuu ya chrismass kwa kutoa misa ya usiku wa manane katika kanisa la mtakatifu Peter Basilica. Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki amewataka watu kutenga muda wao katika amisha yao kwa ajili ya Mungu na watu wenye shida. Benedict akiadhimisha chrismass ya tatu katika uongozi wake , amesoma misa hiyo kwa zaidi ya watu 10,00o ndani ya eneo la Basilica. Amesema ukweli kuwa Yesu alizaliwa katika zizi kutokana na kukosekana nafasi kwa Mariam na Joseph katika maeneo mazuri mjini Jerusalem kunakinzana na hali ya kisasa. Hali ya Chrismass, kiongozi huyo amesema, inampasa kila mtu kutambua giza lililoko duniani ambako watu wengi wamejifungia kwasababu hawataki kumkubali Mwenyezi Mungu ama ujumbe wake. Sherehe hizo zilitangazwa moja kwa moja katika televisheni katika mataifa 42.