1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benghazi: Wauguzi wa Ki-Bulgaria nchini Libya wakata rufaa dhidi ya hukumu ya kifo

18 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCR9

Ile kesi ya ya huko Libya ambako wauguzi watano wa Ki-Bulgaria walihukumiwa adhabu ya kifo sasa imewasilishwa mbele ya mahakama ya rufaa. Kwa mujibu wa mawakili wa wauguzi hao, hakimu atatoa uamuzi wake mnamo miezi mitatu. Pia daktari wa Kipalastina ambaye naye pia amehukumiwa adhabu ya kifo jana aliwasilisha ombi la kutaka hukumu hiyo isikilizwe tena na mahakama ya rufaa. Raia hao wa kigeni wanatuhumiwa kwamba waliwaambukiza watoto 400 wa Kilibya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi katika hospitali ya huko Benghazi. Lakini mabingwa wanadai kwamba kuzuka ugonjwa huo wa AIDS kunatokana na hali mbaya sana ya uchafu katika hospitali hiyo. Inadaiwa ugonjwa huo ulikuweko miaka minane kabla ya kuwasili raia hao wa kigeni.