1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Hali ya usalama Ujerumani imedhibitiwa.

12 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2z

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ujerumani imesema hali ya usalama haijafanyiwa marekébisho hata baada ya kutolewa taarifa kwamba magaidi wamekamilisha mipango yao ya kushambulia raia wa Marekani nchini humu.

Msemaji wa wizara hiyo amesema hakuna jambo lolote jipya lililoibuka kutokana na taarifa.

Msemaji huyo alikuwa akijibu taarifa ya shirika la habari la ABC la Marekani kwamba maafisa wa Marekani na Ujerumani wanaamini kuna uwezekano mkubwa wa wanajeshi au watalii wa kimarekani kushambuliwa.

Msemaji huyo alisema taarifa hiyo ilizungumzia onyo lililotolewa na Marekani mwishoni mwa mwezi uliopita kwa raia wake walioko Ujerumani.