1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Madereva wa treni wagoma tena Ujerumani

8 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C796

Madereva wa treni nchini Ujerumani hii leo watagoma tena.Kwa mujibu wa chama cha madereva wa treni-GDL,safari hii mgomo huo utadumu saa 42:yaani kuanzia saa sita mchana leo Alkhamisi hadi saa kumi na mbili asubuhi siku ya Jumamosi. Chama cha GDL kimekataa mwito uliotolewa na shirika la reli la Ujerumani-Deutsche Bahn, kurejea kwenye majadiliano mapya.

Inakadiriwa kuwa mgomo wa hii leo utasababisha hasara ya hadi Euro milioni 50 kwa shirika la reli la Ujerumani na huenda ukaathiri kazi katika viwanda vingi.

Madereva wa treni wa GDL wamesema,wataendelea kugoma juma lijalo ikiwa shirika la Deutsche Bahn halitotoa pendekezo jipya la kuwaongezea mishahara.Madereva hao wanadai nyongeza ya asilimia 30.