1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Mazungumzo ya mradi wa nyuklia wa Korea Kaskazini kurejewa mwezi huu

18 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZt

Mazungumzo ya pande sita kuhusu mpango wa Korea Kaskazini wa nishati ya nyuklia yatarejewa mwezi huu, kwa mujibu wa Christopher Hill ambaye ni mwakilishi wa Marekani.

Christopher Hill amekuwa na mikutano kadhaa kwa siku mbili zilizopita mjini Berlin kati yake na Kim Kye-Gwan wa Korea Kaskazini.

Mwakilishi huyo wa Marekani baadaye aliyasifu mashauriano hayo lakini akasema wakati umewadia kwa Korea Kaskazini kutoa uamuzi mwafaka.

Christopher Hill alisema:

“Marekani imeeleza kinaga ubaga haina nia ya kuishambulia Korea Kaskazini. Vinginevyo tunatarajia kuwa na uhusiano mzuri na Korea Kaskazini ambayo haitakuwa na silaha za kinyuklia”

Korea Kaskazini ilijiondoa kwenye mazungumzo ya pande sita mwishoni mwa mwaka elfu mbili na tano baada ya hatua ya Marekani ya kuchunguza fedha za taifa hilo la kikomunisti.