1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel akutana na Sarkozy

12 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJg

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani leo anatazamiwa kukutana na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa mjini Berlin kwa mazungumzo.

Mkutano huo unafuatia ziara ya viongozi hao wawili nchini Marekani.Mpango wa nuklea wa Iran unatazamiwa kuwa juu kwenye agenda.Merkel amesema baada ya kukutana na Rais George W. Bush wa Marekani wiki iliopita kwamba vikwazo zaidi dhidi ya Iran vizingatiwe tu iwapo hakuna dalili ya maendeleo katika mazungumzo na Iran wakati Sarkozy amesema kuna haja ya nchi hiyo kuwekewa vikwazo vikali zaidi.

Viongozi hao pia wanatarajiwa kujadili suala la kujumuisha wahamiaji kwenye jamii na kufanya ziara kwenye shule mjini Berlin. Merkel amekaririwa akisema kwamba nchi hizo mbili zote zinakabiliwa na changamoto moja juu ya suala hilo.

Waziri Mkuun wa Ufaransa Francois Fillon na mawaziri wengine wa serikali zao pia watahudhuria mkutano huo kama sehemu ya mkutano wa kawaida wa mashauriano kati ya Ujerumani na Ufaransa.