1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Msaada wa dharura kwa wahanga wa mafuriko

6 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUV

Ujerumani imetoa msaada wa dharura wa Euro 25,000 kuwasaidia watu walioathirika na mafuriko katika mji mkuu wa Indonesia,Jakarta.Ofisi ya wizara ya mambo ya kigeni mjini Berlin imesema,pesa hizo zitatumiwa na mashirika ya misaada ya Kijerumani nchini Indonesia,kuwapatia wahanga hao maji safi,vyakula vya watoto na kutoa huduma za kimatibabu.Hadi hivi sasa,watu wapatao 40,000 wameshatibiwa kwa maradhi mbali mbali.