1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani yakana kuendesha jela za siri za Marekani.

7 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5L

Serikali ya Ujerumani imekana madai kuwa shirika la ujasusi la Marekani CIA limekuwa likiendesha jela za siri nchini humo.

Madai hayo yalitolewa na kundi la kutoa mbinyo wa kisheria la Uingereza , Reprieve, ambalo linawakilisha wafungwa ambao wanashikiliwa katika jela ya kijeshi ya Marekani huko Guantanamo Bay, Cuba.

Kundi la Reprieve , limesema kuwa linaushahidi kutoka kwa wafungwa watatu ambao wanafahamu kuwa watuhumiwa wanashikiliwa ama wanahamishwa kupitia vituo vya kijeshi vya Marekani nchini Ujerumani.

Reprieve linakiri kuwa halina ushahidi kuweza kuunga mkono madai hayo, lakini linaitaka serikali ya Ujerumani kufanya uchunguzi.

Mwezi uliopita rais George Bush wa Marekani amekiri kuwa CIA imewahoji watuhumiwa kadha katika maeneo ya siri nchi za nje. Hakusema ni wapi.