1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Ujerumani yakataa kutimiza masharti ya wateka nyara.

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCH1

Muda uliowekwa na wateka nyara nchini Iraq ambao wanawashikilia raia wawili wa Ujerumani umepita , lakini serikali mjini Berlin inakataa kutimiza madai ya wateka nyara hao.

Kundi la kigaidi ambalo halijulikani sana linatishia kuwauwa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 61 pamoja na mwanae wa kiume kwa madai kuwa Ujerumani iondoe majeshi yake kutoka Afghanistan.

Mjini Roma siku ya Jumanne, kansela Angela Merkel alirudia msimamo wake kuwa Ujerumani haitasalim amri kwa madai hayo.

Hata hivyo, ameongeza kuwa serikali yake inafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa mateka hao wanaachwa huru.

Hannelore Krause mzaliwa wa mjini Berlin na mwanae wa kiume walikamatwa wiki sita zilizopita wakati watu wenye silaha walipoingia nyumbani mwao mjini Baghdad, ambako amekuwa akiishi kwa muda wa miaka zaidi ya 20.