1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani yasema itaahirisha uamuzi wa kupeleka ndege ya kivita Afrghanistan.

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCb7

Serikali ya Ujerumani imesema itaahirisha uamuzi wake wa kupeleka kusini mwa Afghanistan ndege ya kuchunguza makombora mpaka baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa NATO majuma mawili yajayo.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier amekanusha madai yaliyotolewa na kiongozi wa chama cha Social Democratic bungeni Peter Struck kwamba ndege sita zitapelekwa nchini Afghanistan kusaidia majeshi ya NATO.

Wakati huo huo polisi wa Afghanistan wamesema shambulizi la angani la majeshi ya NATO limesabababisha vifo vya wanamgambo zaidi ya kumi na sita wa Taliban na raia kumi na watatu.

Shambulizi hilo lilitekelezwa jana katika wilaya ya Garamsir katika jimbo la Helmand.