1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani yasherehekea siku kuu ya muungano wa taifa

3 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6b

Ujerumani inasherehekea siku kuu ya muungano wa taifa hii leo ambapo sasa ni mwaka wa 16 tokea lililokuwa eneo ya kikoministi upande wa mashariki kujiunga na upande wa magharibi na kuwa taifa mmoja.

Ma mia ya maelfu ya watu wanatarajiwa kuwasili katika mji wa Kiel kaskazini mwa nchi ambako sherehe kabambe zimepangwa kufanyika, wakihudhuria pia rais Horst Köhler na Kansela Angela Merkel.

Lakini waziri wa maendeleo kwa ajili ya eneo la mashariki mwa Ujerumani, amesema kwamba ingawaje kuna maendeleo fulani yameshafikiwa, hata hivyo eneo la mashariki litahitaji misaada ya kifedha kutoka eneo la magharibi kwa muda wa miaka kati ya 15 na 20 ijayo.