1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Umoja wa Ulaya kuombwa kurefusha muda wa Uturuki kutimiza masharti.

5 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCmK

Ujerumani na Ufaransa zinatarajiwa kuuomba umoja wa Ulaya kuweka muda mwingine wa mwisho kwa Uturuki kufungua bandari na viwanja vya ndege kwa vyombo vya usafiri vya Cyprus.

Hiyo inatarajiwa kuwa moja kati ya mada muhimu wakati kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Jacques Chirac wanatakapokutana leo katika mji wa Mettlach ulioko magharibi ya Ujerumani.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuamua Jumatatu ijayo juu ya kuilazimisha Uturuki kwa kushindwa kufikia mahitaji ya makubaliano ya kufungua bandari na viwanja vya ndege kwa Cyprus, ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

Kufuatia mazungumzo yao , Merkel na Chirac watakutana na rais wa Poland Lech Kachinski kujadili uhusiano na Urusi.

Mkutano huo unafanyika chini ya wiki mbili baada ya Poland kuzuwia mazungumzo kuhusu ushirikiano mpya baina ya umoja wa Ulaya na Urusi, ikisema kuwa inaitaka Urusi kuondoa marufuku iliyowekwa dhidi ya mauzo ya nyama nchini Urusi kwanza.