1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Vikosi vya Ujerumani Afghanistan kujadiliwa

29 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeF

Kiongozi wa chama kinachounda serikali tawala ya mseto nchini Ujerumani cha Social Demokratik Kurt Beck amesema yuko tayari kujadili suala la kuendelea kuwekwa kwa vikosi vya Ujerumani nchini Afghanistan.

Ujerumani hivi sasa inatowa mchango wake kwa shughuli za Umoja wa Kujihami wa Mataifa ya Magharibi NATO nchini Afghanistan kwa kutowa wanajeshi wake kwa Kikosi cha Kimataifa cha Usaidizi wa Usalama ISAF nchini humo,ndege aina ya Tornado na vikosi maalum.

Uwekaji wa kikosi hicho maalum cha KSK umekuwa suala la mjadala ndani ya serikali ya mseto.

Mamlaka ya shughuli hizo yanatazamiwa kuthaminiwa upya na bunge la Ujerumani wakati litapokutana tena baada ya mapumziko ya kiangazi.