1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wabunge wa Ujerumani kujadili pendekezo la NATO

22 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChM

Ujerumani inajadili pendekezo la NATO kutuma ndege za kivita nchini Afghanistan. Wabunge wa Ujerumani wamegawanyika kuhusu pendekezo hilo.

Msemaji wa sera za kigeni wa chama cha kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel, Eckart von Klaeden, anasema ndege hizo zina ruhusa ya bunge la Ujerumani kuruka katika eneo la kaskazini mwa Afghanistan ambako kuna utulivu.

Lakini wanasiasa wengine wanasema bunge linatakiwa liulizwe tena kwa sababu ndege hizo zinaweza pia kutumiwa katika eneo la kusini ambako majeshi ya NATO yanakabiliwa na upinzani mkali wa wapiganaji wa kundi la Taliban.