1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Wafanyakazi wa simu wagoma.

11 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC34

Nchini Ujerumani wafanyakazi 10,000 wa shirika la simu DeutscheTelekom wanafanya mgomo ulioitishwa na chama cha wafanyakazi cha Ver.di kuhusiana na mpango wa shirika hilo wa kuziondoa nafasi za kazi 50,000 na kuzipeleka nje ya shirika hilo.

Msemaji wa chama cha wafanyakazi cha Ver.di Lothar Schröder amedai kuwa mpango huo wa kuzipeleka nafasi hizo za kazi nje ya shirika hilo ufutwe.

Deutsche Telekom inapanga kutengeneza huduma mpya zenye ufanisi kwa wateja kutokana na nafasi hizo 50,000 , ambapo wafanyakazi watafanyakazi kwa masaa mengi kwa malipo madogo.

Mkuu wa shirika la Telekom Rene Obermann amekitaka chama cha Ver.di kuingia katika majadiliano.

Mvutano huo unaingiliana na hasara iliyopata shirika hilo katika robo ya kwanza ya mwaka huu. Matatizo ya Telekom kwa kiasi kikubwa ni kutokana na kuondoka kwa kiasi cha wateja zaidi ya nusu milioni , na kupata huduma kwa mashirika mengine rahisi, ambayo ni washindani wa huduma za simu wa Telekom.