1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wanamgambo waionya Ujerumani kwenye mtandao

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCK3

Serikali ya Ujerumani imesema,wataalamu wanachunguza risala mbili za kanda za video zilizowekwa kwenye mtandao wa Internet, unaosemekana kuwa ni wa makundi ya kigaidi.Kanda mpya inaonya kuwa Ujerumani na Austria zitakabiliana na mashambulio ya wanamgambo ila kama zitaondosha vikosi vyao kutoka Afghanistan. Kanda hii inafuata ile iliyotolewa siku ya Jumamosi.Katika kanda hiyo wanamgambo wa Kiiraki wameonekana wakimshikilia mwanamke wa Kijerumani pamoja na mwanae wa kiume na kutishia kuwaua isipokuwa Berlin itaondosha vikosi vyake kutoka Afghanistan katika kipindi cha siku 10.Serikali ya Ujerumani ina kama wanajeshi 3,000 nchini Afghanistan.Vikosi hivyo ni sehemu ya majeshi ya kimataifa yanayolinda usalama nchini humo chini ya uongozi wa NATO.