1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Washambulizi wa Taasisi ya Goethe waadhibiwe

30 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFHv

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Joschka Fischer amesema shambulio lililofanywa dhidi ya Taasisi ya kujifunza lugha ya Kijerumani-Goethe Institute nchini Togo ni kitendo cha fujo,kisicho halali na kisichokubalika.Fischer ametoa wito kwa serikali mjini Lome ifanye iwezavyo kuwakamata na kuwaadhibu wahusika.Amesema,serikali inapaswa kuhakikisha kuwa inawalinda vya kutosha Wajerumani na taasisi za Kijerumani nchini Togo.Vile vile kampeni dhidi ya Wajerumani isitishwe.Usiku wa Ijumaa, Taasisi ya Goethe katika mji mkuu Lome,ilishambuliwa na kutiwa moto na watu waliobeba silaha.Serikali ya Togo imeituhumu Ujerumani kuwa imeuunga mkono upande wa upinzani katika mgogoro wa uchaguzi wa rais.