1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Waziri wa Nje wa Ujerumani ziarani Ghana

3 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBci

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier hii leo anamaliza ziara yake ya siku tatu katika Afrika ya Magharibi.Akiwa katika kituo cha pili cha ziara hiyo katika mji mkuu wa Ghana,Accra waziri Steinmeier hii leo atatembelea Taasisi ya Kofi-Annan inayotoa mafunzo kwa tume za amani.Ujerumani,imetoa msaada wa kama Euro milioni sita,tangu kituo hicho cha mafunzo kuzinduliwa katika mwaka 2002.

Siku ya Alkhamisi,Steinmeier alikutana na Rais wa Ghana,John Kufour ambae hivi sasa ameshika wadhifa wa rais katika Umoja wa Afrika.Mkutano huo ulihudhuriwa pia na waziri wa mambo ya nje wa Ghana,Osei Adjei.Hapo awali Steinmeier alikuwepo Nigeria.