1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wito kurefusha ujumbe wa Afghanistan

21 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBO1

Waziri wa Masuala ya Nje,Frank-Walter Steinmeier na Waziri wa Ulinzi,Franz Josef Jung wa Ujerumani,wametoa mwito kwa wabunge mjini Berlin kutoa idhini ya kurefusha ujumbe wa kijeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan.

Mawaziri hao walikuwa wakizungumza wakati wa mdahalo wa kuendelea kubakisha wanajeshi 3,000 kulinda amani nchini Afghanistan,kama sehemu ya majeshi ya kimataifa,chini ya uongozi wa NATO na vile vile kubakisha ndege sita za upelelezi aina ya Tornado.Serikali ya mseto ya Kansela Angela Merkel ina uwingi mkubwa bungeni.Inatazamiwa kuwa ujumbe wa Ujerumani nchini Afghanistan, utarefushwa katika kura itakayopigwa mwezi ujao.