1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Brown ziarani Ujerumani

17 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhm

Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amewasili nchini Ujerumani jana usiku ikiwa ni ziara yake ya kwanza rasmi toka alipochukua madaraka wiki tatu zilizopita.

Brown ambaye alipokewa na Kasela wa Ujerumani Angela Merkel alimsifu kansela huyo kwa mchango wake katika kufikiwa kwa makubaliano juu ya mkataba mpya wa Umoja wa Ulaya mwezi uliyopita mjini Brussels.

Pia Gordon Brwon alisema kuwa Uingereza huenda ikapitia upya uamuzi wake wa kutokuwa mshirika wa fedha ya euro ambayo wiki iliyopita ilizidi kupanda thamani dhidi ya Dola ya Marekani.

Mbali ya kuzungumzia majaaliwa ya Umoja wa Ulaya, pia viongozi hao walisema kuwa mazungumzo yalijikita katika masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, vita dhidi ya ugaidi na kupambana na umasikini barani Afrika.