1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:India yaitaka Ujerumani ilinde raia wake wanaoishi Ujerumani

22 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBX1

India imeitaka serikali ya Ujerumani ichukue hatua za kuwalinda raia wa kihindi wanaoishi nchini Ujerumani.

India imesema hayo katika tamko lililotolewa na wizara yake ya mambo ya nje kufuatia mkasa uliotokea jumamosi iiyopita, ambapo wahindi wanane walishambuliwa katika jimbo la Saxony mashariki mwa Ujerumani.

Wahindi hao walishambuliwa na kundi la vijana 50 wa kijerumani wanaotuhumiwa kuwa mafashisti mamboleo.

Wahindi watatu waliumizwa vibaya na wajerumani hao kabla ya polisi kuwasili.