1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin.Kansela Angela Merkel azungunza na Jaroslaw kaczynski.

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxf

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na waziri mkuu wa Poland Jaroslaw Kaczynski wamemaliza mazungumzo yao yaliyohusu mada kuu mbili.

Katika hatua za kusaidia kuwa sambamba na Poland Bibi Merkel ameahidi kupata gesi kutoka Ulaya Magharibi ikiwa usambazaji kutoka Urusi unatishia usalama.

Ahadi yake hiyo imekuja kufuatia mazungumzo yake na waziri mkuu wa Poland ambae amerejea kauli ya Warsaw kupinga mpango wa kutengeneza bomba la gesi litakalopita chini ya bahari ya Baltic litakalopitisha gesi moja kwa moja kutoka Urusi kuelekea nchini Ujerumani.

Akithibitisha kauli yake katika mazungumzo hayo Kansela Angela Merkel alisema.

“Nimeeleza wazi na bila ya upendeleo kwamba kuhusu ujenzi wa bomba la gesi kupitia bahari ya Baltic, Ujerumani kama mwanachama wa Umoja wa Ulaya ni jambo inalolielewa. Kila mradi ulioko Ulaya hauna budi kuwa ni mradi unaoweza kutafutiwa suluhisho na mataifa mengine na sio mradi dhidi ya taifa jengine“.

Mada nyengine iliyozungumzwa katika kikao cha viongozi hao ni kuhusu wasi wasi wa Poland kutokana na madai ya kulipwa fidia Wajerumani waliopokonywa milki zao na kufukuzwa nchini Poland baada ya vita vya pili vya Dunia.

Kansela Angela Merkel alikwishasema hapo awali kwamba serikali yake haiungi mkono madai yanayotolewa na makundi kama hayo ya watu.