1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Kansela Merkel aahidi kufufua mchakato wa katiba ya Umoja wa Ulaya

12 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3h

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema kuwa serikali yake inakusudia kufanya juhudi ili katiba ya Umoja wa Ulaya ipitishwe.

Ujerumani itakuwa rais wa Umoja wa Ulaya kwa muda wa miezi sita kuanzia mwezi wa januari mwaka ujao.

Bibi Merkel amesema, katika kipindi hicho serikali yake itatekeleza mpango maalumu, ili katiba ya Umoja huo ipitishwe.

Katiba hiyo haikuweza kuidhinishwa na nchi za Ulaya baada ya idadi kubwa ya wananchi wa Ufaransa na Uholanzi kuikataa katika kura za maoni zilizofanyika mwaka jana.