1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mjerumani atekwa nyara Afganstan

4 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlz

Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imesema raia mmoja wa Ujerumani ametekwa nyara nchini Afghanstan hii leo.Msemaji wa wizara hiyo mjini Berlin Martin Jaeger amewambia waandishi wa habari kwamba raia wa Ujerumani alitoweka tangu siku ya alhamisi iliyopita nchini Afghanstan na kwamba maofisa wanaamini ametekwa nyara.

Mjerumani huyo aliyetekwa nyara inaaminika sio mwanajeshi wala mwandishi habari au mfanyikazi wa shirika fulani.Hata hivyo hadi sasa hakuna maelezo zaidi yaliyoweza kutolewa kwa haraka.