1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mkakati mpya wa Bush wakaribishwa

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuz

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameukaribisha mkakati mpya wa rais George Bush wa Marekani kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani lakini ametahadharisha kuwa mkakati huo ni lazima uambatane na itifaki ya mjadala wa umoja wa mataifa.

Bibi Merkel aliyasema hayo wakati alipowahutubia waandishi wa habari baada ya kukutana na waziri mkuu wa Uingereza anaendoka Tony Blair.

Bwana Blair alisema kuwa analiunga mkono pendekezo la kansela Angela Merkel wa Ujerumani.

Bibi Merkel amesema swala la mabadiliko ya hali ya hewa duniani ndilo litakuwa la muhimu zaidi katika mkutano wa siku tatu wa viongozi wa kundi la mataifa tajiri kiviwanda G8 katika mji wa Heiligendamm hapa nchini Ujerumani.

Wakati huo huo polisi hapa nchini Ujerumani imearifu kuwa takriban watu 1000 walijeruhiwa katika maandamano ya mwishoni mwa wiki ya kupinga mkutano wa kilele wa G8 yaliyofanyika katika mji wa kaskazini wa Rostock karibu na mahala patakapofanyika mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa G8.

Waandalizi wa maandamano hayo wametuhumu vikali ghasia hizo.

Ulinzi umeimarishwa zaidi katika maeneo ya kuelekea mahala patakapofanyika mkutano huo wa kilele.

Watu 128 wamekamatwa kufuatia ghasia hizo, takriban waandamanji 520 na polisi 433 walijeruhiwa katika ghasia hizo.