1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:M´tu anayeshukiwa kuwa mpelelezi wa Sudan akamatwa

23 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7DJ

Maafisa nchini Ujerumani wamemkamata mtu mmoja anayeshukiwa kuwa mpelelezi wa serikali ya Sudan ambaye amekuwa akipeleka taarifa kwa shirika la upelelezi la Sudan juu ya shughuli za wafuasi wa Upinzani walioko Ujerumani.

Afisi ya mshtaki mkuu wa serikali imesema mtu huyo mwenye umri wa miaka 39 alikamatwa mjini Berlin mwishoni mwa juma lakini taarifa hizo zimetolewa leo.

Inadaiwa mtu huyo ameanza kufanya shughuli hiyo ya upelelezi tangu mwezi juli mwaka 2005.