1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Ujerumani kutafakari jukumu la jeshi lake nchini Afghanistan

5 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBST

Baraza la mawaziri la Ujerumani leo linatafakari jukumu la kulinda amani linalotekelezwa na wanajeshi wa Ujerumani nchini Afghanistan.

Ujerumani inakusudia kuimarisha kazi za ujenzi mpya kwa kuongeza msaada wa fedha hadi kufikia Euro milioni 125.

Kwengineko waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora anakutana leo hii na kansela Angela Merkel wa Ujeruman mjini Berlin.

Baadae waziri mkuu wa Lebanon atakutana pia na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmier na waziri wa maendeleo bibi Heidemarie Wieczorek-zeul.