1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Ujerumani yamtaka Gadaffi kufafanua juu ya madai ya mwanaye

11 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaD

Ujerumani imemtaka kiongozi wa Libya Kanali Mohammar Gadaffi kutoa ufafanuzi kufuatia kauli iliyotolewa na mtoto wake ya kwamba wauguzi sita wa Bulgaria waliteswa walipokuwa katika jela za nchi hiyo.

Mtoto huyo wa Gadaffi, aitwaye Saif al Islam ambaye alisadia katika muafaka wa kuachiwa kwa wauguzi hao mwezi uliyopita alikiri katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Jazeera ya kwamba wauguzi hao pamoja na daktari mmoja wa kipalestina waliteswa wakati wa mahojiano.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Gernot Erler akinukuliwa na gazeti la Tagesspiegel la hapa Ujerumani alisema kuwa serikali ya Libya na Kanali Gadaffi wathibitishe kama kauli hiyo ya mtoto wake ni kweli au la.