1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biashara ya silaha yapungua duniani, ila Urusi

15 Desemba 2014

Makampuni ya ulinzi nchini Marekani na Ulaya ya magharibi yamekamata mstari wa mbele katika biashara ya silaha mwaka 2013 kwa mujibu wa ripoti ya taasisi ya uchunguzi wa masuala ya amani ulimwenguni-SIPRI.

https://p.dw.com/p/1E4CG
Nembo ya taasisi ya kimataifa inayochunguza masuala ya amani-SIPRI

Biashara ya vifaa vya kijeshi na huduma iliyofanywa na makampuni 100 makubwa ya silaha imefikia jumla ya dala bilioni 402, ikipungua kwa asili mia mbili ikilinganishwa na mwaka 2012-taasisi ya SIPRI imesema katika ripoti yake.

Miongoni mwa makampuni 100 makubwa yaliyoorodheshwa,38 yana makao yake nchini Marekani,moja nchini Canada na 30 katika nchi za Ulaya ya Magharibi.Kwa pamoja makampuni hayo yanafikia asili mia 85 ya biashara jumla ya silaha kwa mwaka 2013.

Biashara kutoka makampuni 10 ya silaha ya Urusi yaliyoorodheshwa na SIPRI, inafikia jumla ya dala bilioni 31,ikiongezeka kwa asili mia 20 ikilinganishwa na mwaka 2012.Kampuni kubwa zaidi la silaha la Urusi Almaz Antei linakamata nafasi ya 12 ikilinganishwa na nafasi ya 14 mwaka 2012.

Urusi imepania kujiimarisha kijeshi

Pato jumla limepungua mwaka 2013-kwa mara ya tatu mfululizo,na kusalia kuwa chini kuliko la mwaka mmoja kabla kutokana na kuongezeka biashara ya silaha kutoka Urusi na kuongezeka mahitaji kutoka Brazil,India,Korea ya kusini na Uturuki miongoni mwa nchi nyenginezo.

Infografik Die fünf größten Waffenexporteure SIPRI 2013 RUS russisch
Ramani (ya mwaka 2013) ya madola matano yanayosafirisha silaha kwa wingi duniani (

Makampuni ya China hayahusiki na hesabu hizo kuitokana na ukosefu wa maelezo kuhusu biashara ya silaha ya nchi hiyo.Taasisi hiyo ya mjini Stockholm inayaochunguza masuala ya amani ulimwenguni imesema katika ripoti yake huenda makampuni tisaa ya China yakakutikana miongoni mwa mia moja yanayouza silaha.

Kuongezeka biashara ya silaha nchini Urusi kunatokana na kuongezeka biashara ya nje pamoja na kuimaarishwa mnamo miaka ya hivi karibuni makampuni kadhaa ya silaha yanayomilikiwa au yanayosimamiwa na serikali-mtaalam wa taasisi ya SIPRI,Siemon Wezeman amesema katika mahojiano na shirika la habari la Ujerumani dpa.

"La muhimu kabisa ni kwamba bajeti ya kijeshi ya Urusi inaongezeka" amesema na kuongeza tunanukuu:"Urusi imepania kuvigeuza vikosi vyake viwe vya kimambo leo."Mwisho wa kumnukuu.

Miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya silaha nchini Urusi ni pamoja na kurekebisha vifaa na nguvu kazi na pia suala kama Urusi itamudu kuendelea na mipango mikubwa mikubwa na ghali ya ulinzi,kuanzia nyambizi,kupitia ndege za kivita hadi kufikia silaha ndogo ndogo.

Ushirikiano pamoja na nchi nyengine,ikiwa ni pamoja na China na India ni mojawapo ya mikakati.

Lockheed Martin na Boeing ya Marekani yanaongoza

Kuondoshwa vikosi vya Marekani nchini Afghanistan na Irak ni mojawapo ya sababu za kupungua kwa asili mia 4.5 biashara ya silaha ya Marekani.Hata hivyo makampuni 6 ya Marekani yameorodheshwa miongoni mwa makampuni kumi makubwa ikiwa ni pamoja na lile Lockheed Martin linaoongoza orodha hiyo na kufuatiwa na Boeing.

Bildergalerie Mächtigste Managerinnen 7 Marillyn Hewson
Marillyn Hewson meneja wa kampuni kubwa ya silaha ya Marekani ya Lockheed MartinPicha: Getty Images

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/düpa/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu