1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bibi Livni mbioni kujaribu kuunda serikali Israel.

19 Oktoba 2008
https://p.dw.com/p/Fd0W

Jerusalem:

Kiongozi mpya wa chama cha Kadima nchini Israel Bibi Tzipi Livni anatarajiwa kuimarisha juhudi za kuunda serikali mpya ya muungano na kuwa Waziri mkuu wa Israel, baada ya muda wa siku 28 za awali wa kuunda serikali kumalizika hapo kesho (Jumatatu).

Bibi Livni ambaye ni waziri wa mambo ya nchi za nje amekua akijaribu kuunda serikali ya mseto na vyama vyengine, tangu alipochaguliwa kukiongoza chama cha Kadima mwezi uliopita, kuchukua nafasi ya Bw Ehud Olmert aliyejiuzulu Uwaziri mkuu kutokana na kashfa ya rushwa. Huenda Bibi Livni akakutana na Rais Shimon Perez kesho kuomba majuma mawili zaidi kama anavyoruhusiwa kikatiba, ili ajaribu kuunda serikali.