1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamfalme anataka uchaguzi ufanyike haraka

14 Oktoba 2015

Mgombea wa urais katika shirikisho la soka duniani Fifa mwana mfalme Ali Bin al-Hussein anasema kuwa kucheleweshwa kokote kwa uchaguzi wa kumteua mrithi wa Sepp Blatter kutaliyumbisha zaidi shirikisho hilo

https://p.dw.com/p/1GoUB
FIFA Präsidentschaft Kandidat Ali Bin al Hussein
Picha: Getty Images

Raia huyo wa Jordan anapanga kuchukua mikoba ya Sepp Blatter aliyesimamishwa uongozi kwa mda wa siku 90 katika uchaguzi wa mwezi Februari.

Lakini Blatter mwenye umri wa miaka 79 pamoja na rais wa Shirikisho la Vyama vya Kandanda barani Ulaya - UEFA Michel Platini walisimamishwa kazi kwa mda wa siku 90 huku FIFA ikitarajiwa kujadiliana kuhusu kuahirisha uchaguzi huo.

Blatter na Platini wote wameenda mahakamani kupinga hatua hiyo ya kamati ya maadili ya FIFA.

Katibu mkuu Jerome Valcke pia amesimamishwa kazi. Wote watatu wamekana kufanya uovu wowote.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Abdulrahman