1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bingwa Italia yatimuliwa

Martin,P/ZPR25 Juni 2010

Italia iliyokuwa ikitetea taji lake, imepigwa kumbo katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/O2gb
epa02220156 Italian player Fabio Cannavaro (L) consoles teammate Fabio Quagliarella after the FIFA World Cup 2010 group F preliminary round match between Slovakia and Italy at Ellis Park stadium in Johannesburg, South Africa, 24 June 2010. Italy lost 2-3. EPA/KERIM OKTEN Please refer to www.epa.eu/downloads/FIFA-WorldCup2010-Terms-and-Conditions.pdf
Mchezaji wa Italia,Fabio Cannavaro (kushoto) akimtuliza mwenzake Fabio Quagliarella, baada ya mabingwa wa 2006 Italia kufungishwa virago na Slovakia.Picha: picture-alliance/dpa

Mabingwa hao wa mwaka 2006 wamefungishwa virago na Slovakia baada ya kucharazwa mabao 3-2 walipokumbana hiyo jana kwenye uwanja wa Ellis Park mjini Johannesburg.

Katika mchezo mwingine wa kuamua nani atakaesonga mbele na kuingia duru ya pili ya michuano hiyo,Paraguay iliyopambana na New Zealand, imejipatia tikti ya kubakia katika michuano hiyo, licha ya pande hizo mbili kutoka uwanjani bila ya kumpachika mwenzake hata goli moja.

Netherlands' Wesley Sneijder, left, and Cameroon's Landry Nguemo vie for the ball during the World Cup group E soccer match between Cameroon and the Netherlands in Cape Town, South Africa, Thursday, June 24, 2010. (AP Photo/Schalk van Zuydam)
Wesley Sneijder wa Uholanzi (kushoto) na Landry Nguemo wa Cameroon wakiugombea mpira katika michuano ya Kombe la Dunia.Picha: AP

Na Uholanzi imeifunga Cameroon mabao 2-1 na hivyo imeingia katika duru ya pili bila ya kushindwa katika michezo yake yote mitatu.

Japan nayo hiyo jana, katika mchezo wa kufa kupona, iliikandika Denmark mabao 3-1 na hivyo imejipatia tikti ya kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.