1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blackwater lahusishwa na magendo nchini Iraq

23 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNL

Washington:

Shirika la Usalama la Marekani Blackwater limekanusha madai ya kuhusika na mitindo ya kuingizwa silaha kinyume na sheria nchini Iraq.”Tuhuma kama hizo hazina msingi”-limesema shirika hilo katika taarifa yake.Kwa mujibu wa ripoti zilizochapishwa na shirika la habari la AP,wanasheria nchini Marekani wanachunguza ripoti zianzodai watumishi wa shirika la Blackwater wamekua wakiingiza silaha kinyume na sheria nchini Iraq na kuziuza baadae kimagendo.Shirika hilo la usalama limekua likikoselewa tangu watumishi wake walipofyetua risasi na kuwauwa wairaq wasiopungua kumi hivi karibuni mjini Baghdad.