1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blair ahojiwa kuhusu Iraq

Sekione Kitojo30 Januari 2010

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ametetea uamuzi wake wa kushiriki katika uvamizi dhidi ya Iraq ulioongozwa na Marekani katika mwaka 2003.

https://p.dw.com/p/LnP2
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ambaye alihojiwa siku ya Ijumaa kwa kuhusika kwake na uvamizi dhidi ya Iraq.Picha: AP

LONDON:

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ametetea uamuzi wake wa kushiriki katika uvamizi wa Iraq ulioongozwa na Marekani katika mwaka 2003. Akizungumza mbele ya tume inayochunguza sababu za kuingia vita vya Iraq,Blair alisema kuwa hajuti kusaidia kumuondosha madarakani kiongozi wa Iraq Saddam Hussein. Amesema kufuatia shambulio la kigaidi la Septemba 11 nchini Marekani, ilikuwa dhahiri kuwa serikali zenye silaha za maangamizi zisistahimiliwe tena. Uchunguzi unaofanywa hivi sasa unataka kujua iwapo Blair alikuza ripoti za upelelezi zilizodai kuwa Iraq ilikuwa na silaha za maangamizi na iwapo uvamizi wa Iraq umekiuka sheria ya kimataifa.