1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BLANTYRE : Serikali ya Malawi yumkini kusambaratika

15 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrW

Mahkama Kuu nchini Malawi leo hii imempa madaraka spika wa bunge kuwatimuwa wabunge wanaoasi vyama vyao katika hatua ambayo yumkini ikapelekea kusambaratika kwa serikali ya Rais Bingu wa Mutharika yenye viti vichache bungeni.

Katika hukumu ambayo ilikuwa ikitarajiwa sana Hakimu Mkuu Leonard Unyolo ameamuwa kwamba spika anaweza kutumia kifungu cha kumtimuwa mbunge yoyote yule ambaye amebadili ufuasi wa vyama wakiwemo wabunge 30 wa upinzani na wa kujitegemea ambao hivi sasa wanakalia viti vya serikali.

Takriban wabunge 60 kati ya wabunge 193 wataathiriwa na hukumu hiyo nusu yake wakiwa ni wafuasi wa serikali ya Mutharika na chama chake tawala cha Demokratic Progress.