1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blatter, Platini wapigwa marufuku na FIFA

Admin.WagnerD21 Desemba 2015

Rais wa FIFA Joseph Sepp Blatter na rais wa UEFA Michel Platini wamepigwa marufuku kushiriki shughuli zozote za kandanda kwa miaka minane, na kamati ya maadili ya shirikisho hilo kandanda duniani

https://p.dw.com/p/1HRHH
Michel Platini und Joseph Blatter
Picha: picture-alliance/dpa/M. Brandt

Viongozi hao wamepigwa marufuku kushiriki shughuli zozote za mpira wa miguu kitaifa na kimataifa mara moja, imesema kamati hiyo ya FIFA.

Kamati hiyo imefikia maamuzi kwamba kulikuwa na ukiukaji wa maadili yanayohusiana na "ulipaji fedha kinyume na utaratibu" wa kiasi cha fedha za Uswisi Francs milioni 2 zilizolipwa kwa Platini mwaka 2011.

Marufuku hayo dhidi ya Blatter na Platini yanafikisha mwisho kipindi chake cha uongozi wa kandanda pamoja na matumaini ya Platini ya kumrithi kama rais wa FIFA.

Blatter na Platini walikuwa wamesimamishwa kufanya shughuli za uongozi kwa kipindi cha siku 90 Oktoba 8 mwaka huu kwa kuhusika na malipo hayo, ikiwa ni sawa na kiasi cha karibu dola milioni 2, alizopokea Platini mwaka 2011 kwa ajili ya kazi za FIFA zilizofanyika kati ya mwaka 1998 na 2002.

Sepp Blatter katika mkutano na waandishi habari amezungumzia kuhusu makubaliano kama alivyoyaita ya "waungwana" kati yake na Michel Platini kabla ya kulipa fedha hizo. "Tumo katika kile kinachoitwa mkataba wa maneno, ama " makubaliano ya waungwana" na makubaliano haya ya waungwana yalifanyika tayari mwaka 1998, mara tu baada ya fainali za kombe la dunia nchini Ufaransa ambako Bwana Platini alinifuata na nikamfuata kwa kuwa tunafanyakazi pamoja - na alisema alipenda kuifanyia kazi FIFA na nikasema itakuwa vizuri iwapo utakuja FIFA. Alisema " lakini mimi ni mtu ghali, thamani yangu ni francs milioni moja. Nilisema , hiyo ni sawa lakini hatuwezi kukulipa sasa kwasababu hatuwezi kulipa. Tutakulipa sehemu na kisha baadaye. Lakini kile kinachonishangaza hivi sasa, iwapo nitaangalia uamuzi wa kamati hii leo, ni uamuzi wa mwisho lakini , ni kwamba wanakana , wanakana kuwapo kwa makubaliano kama hayo?

Schweiz suspendierter FIFA-Präsident Sepp Blatter
Picha: picture-alliance/dpa/W. Bieri

Blatter alifafanua makubaliano hayo kwa waandishi habari mjini Zurich kufuatia uamuzi wa kumpiga marufuku yeye pamoja na Platini kufanya shughuli zozote zinazohusu kandanda kwa miaka minane. viongozi hao wote wawili wanakana kutenda kinyume na sheria katika mwaka 2011 wakati Platini alipopokea dola milioni 2 fedha za FIFA zilizoidhinishwa na Blatter kama msharara ambao haumo kimkataba kwa kazi kama mshauri wa rais kuazia mwaka 1999 hadi 2002. Shughuli za uongozi wa Blatter katika FIFA unamalizika kwa fedheha baada ya zaidi ya miaka 17 ya urais na miaka 40 kwa jumla ya kufanyakazi katika shirikisho hilo lililokumbwa na kashfa tele.

hata hivyo Sepp Blatter amesema atakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa kamati ya maadili ya FIFA. Akizungumza mjini Zurich katika eneo la makao makuu ya zamani ya FIFA , Blatter amesema kwanza ataipeleka kesi yake katika kamati ya rufaa ya FIFA kabla ya kupambana na uamuzi wa kumsimamisha katika mahakama ya upatanishi katika michezo mjini Lausanne.

Mnaniuliza iwapo nahisi nimesalitiwa , jibu ni ndio, amesema rais huyo wa Uswisi.

wakati huo huo shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA limesema limekatishwa tamaa na uamuzi wa FIFA wa kumpiga marufuku Michel Platini rais wa shirikisho hilo kwa miaka minane kuhusiana na ukiukaji wa maadili , na kuelezea kuunga mkono haki ya raia huyo wa Ufaransa kukata rufaa.

"UEFA inaunga mkono haki ya Platini kupata haki na fursa ya kusafisha jina lake , taarifa ya UEFA imesema.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe / dpae
Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman