1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bobs 2014: DW kutambua kazi za wanaharakati bora wa mtandaoni

Sarah Steffen5 Februari 2014

Wakati watumiaji wa mtandao wa Intaneti wakitafuta njia za kupeana taarifa huku wakilinda faragha zao, tuzo ya Bobs ya DW inatafuta mifano bora ya uwanaharakati wa mtandaoni. Maombi yanaweza kutumwa hadi Machi 5.

https://p.dw.com/p/1B2wi
Tuzo za Bobs za DW zinatambua uwanaharakati bora wa mtandaoni.
Tuzo za Bobs za DW zinatambua uwanaharakati bora wa mtandaoni.

Tangu zilipoanzishwa mwaka 2004, tuzo za Deutsche Welle za uwanaharakati wa mtandaoni "Bobs", zimejikita katika kutambua juhudi zinazofanywa kulinda uhuru wa kujieleza si tu kwa vyombo vya habari, bali pia kwa watu mmoja mmoja duniani kote.

"Kabla ya zama hizi za uunganishwaji, uhuru wa kujieleza ulikuwa ni haki ya wale tu waliokuwa na njia za kutumia vyombo vya habari," alisema Luis Orihuela, mjumbe wa zamani wa jopo la tuzo za Bobs na profesa wa mawasiliano kwa njia tofauti katika Chu Kikuu cha Navarra mjini Pamplona, Uhispania.

"Kuanzia katika mapinduzi ya blogi, uhuru wa kujieleza ni haki inayostahiki kulindwa kwa kila raia kwa sababu simu iliyounganishwa inamuwezesha kila mmoja kuwa sehemu ya habari duniani," Orihuela alisema.

Moja wa majaji wa tuzo za Bobs Alexander Youssef kutoka Brazil.
Moja wa majaji wa tuzo za Bobs Alexander Youssef kutoka Brazil.Picha: privat

Mchezo wa paka na panya

Lakini kutegemea na wapi watu wanaishi, kupeana maoni na ulimwengu limekuwa jambo la hatari wakati ambapo uhuru wa Intanet umepungua duniani kote kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2013 ya shirika la ufuatiliaji la Freedom House. "Tunashuhudia muendelezo wa vurugu dhidi ya wanahabari na waendeshaji wa blogi, ambao dunia inapaswa kuumulika," alisema Hauke Gierow, mkuu wa kitengo cha uhuru wa intanet katika shirika la waandishi wasio na mipaka nchini Ujerumani.

Miaka kumi iliyopita, uchunguzi wa intanet lilikuwa tatizo maarufu nchini China, Iran na katika tawala nyingine za ukandamizaji. Wanaharakati na wapinzani wa serikali, wakifahamu kuwa walikuwa wakifuatiliwa, walilaazimika kuchukua hatua za kuwakwepa wakaguzi wa serikali na kuepuka kujidhihirisha wao na kazi zao kwa mamlaka.

Serikali ya China inakwenda mbali zaidi kuuzuwia umma kuingia katika tovuti na huduma nyingine za mtandaoni inazotaka kuzizuwia, na mchezo wa paka na panya kati ya wakaguzi wa serikali na watu wanaobuni teknolojia ya kuwakwepa umeendelea kwa miongo kadhaa, alisema Gierow. Mradi wa "We Fight Censorship", ambao unaendeshwa na shirika la maripotai wasio na mipaka, unaorodhesha wanaharakati 164 wa mtandaoni walioko gerezani duniani kote.

Upanuzi wa uchunguzi

Hata hivyo, baada ya ufichuaji wa wakala wa zamani wa shirika la usalama wa taifa la Marekani NSA Edward Snowden, imebainika wazi kuwa siyo raia wanaoishi chini ya tawala za kidikteta tu wanaohitaji kuwa na wasiwasi kuhusu haki zao za faragha. Nyaraka alizofichua Snowden zinaonyesha kuwa NSA inaweza miongoni mwa mambo mengine, kufuatilia mawasiliano ya simu, ujumbe mfupi wa maandishi na kuingia katika barua pepe za watu na kukagua historia zao za mawasiliano.

"Ufichuaji wa Snowden unapaswa kutuongoza kuwawajibisha wale wanaoshirikiana na serikali kumchunguza kila mmoja, kudhoofisha mifumo yetu na imani ya watumiaji," alisema Renata Avila, wakili wa haki za binaadamu na haki miliki kutoka nchini Guatemala, ambaye pia ni mjumbe wa jopo la majaji wa Bobs.

Tuzo za Bob za DW mwaka 2014.
Tuzo za Bob za DW mwaka 2014.

Imani iliyovunjika

Wakati watu wengi nchini Marekani na mataifa mengine yanayoongozwa kidemokrasia waliziamini taasisi za serikali kulinda faragha zao, Mjumbe wa jopo la Bobs Arash Abadpour alisema Wairan wamejifunza tayari kwamba wanahitaji kujilinda wenyewe. "Alichokionyesha Snowden ni kwamba imani hii wakati mwignine ni ya kufikirikika," alisema Adapour. "Mara nyingine nashangaa ni ngazi ipi ya imani inatekelezeka."

Lakini hadi aina hiyo imani ijengwe, Avila aliongeza, watu duniani watahitaji kuendelea kutafuta njia za kupeana taarifa wakati wakilinda faragha zao na usalama. "Wakati vyombo vikuu vya habari vikiwa kimya, blogi inayoendesha katika mamlaka mahiri, ikikingwa na ufichaji wa majina ndiyo kiuasumu dhidi ya ukaguzi," alisema.

Bobs inakaribisha maombi

Kuanzia Jumatano (05.02.2014), Mashindano ya Bobs yanatafuta maoni ya watu juu ya miradi inayohamaisha zaidi na kampeni zinazounga mkono uhuru wa kujieleza na uanaharakati wa mtandaoni. Watumiaji wa intaneti duniani kote wana mwezi mmoja kutuma maombi katika moja kati ya lugha 14 za shindano hilo katika tovuti ya www.thebobs.com.

Mwandishi: Sinico, Sean/Steffen Sarah
Tafsiri: Iddi Ismail Ssessanga
Mhariri: Mohamed Abdul-Rahman