1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BOGOTA : Bush kuwasili Colombo

11 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKE

Rais George W. Bush wa Marekani anatazamiwa kuwasili katika mji mkuu wa Colombia Bogota leo hii akiwa katika kituo cha tatu cha ziara yake ya mataifa matano Amerika ya Kusini.

Akiwa nchini Colombia anatazamiwa kuelezea kuendelea kkunga mkono juhudi za nchi hiyo kupambana na uasi wa mrengo wa shoto na usafirishaji haramu ya madawa ya kulevya.

Hata hivyo ziara yake hiyo itakuwa ya masaa sita tu kutokana na wasi wasi kwamba waasi yumkini wakajaribu kuvuruga mkutano wake na Rais Alvaro Uribe wa Colombia kwa kufanya mashambulizi.

Wakati wa ziara yake hii Bush amegoma kujibu vijembe vya Rais Hugo Chavez wa Venezuela ambaye anafanya ziara Amerika ya Kusini sambamba na Bush.Akitembelea Bolivia Chavez amesema ubepari ni barabara ya kuelekea motoni na kumwita Bush kuwa ni mkuu wa hemaya hiyo.

Kwa upande wake Bush ameendelea kushikilia ujumbe wake wa mshikamano na bara hilo.

Ziara ya kiongozi huyo wa Marekani nchini Brazili na Uruguay ilikabiliwa na maandamano ambayo baadhi yake yaligeuka kuwa ghasia.