1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bolt akaribia kutimiza ndoto yake

Bruce Amani
8 Januari 2018

Mwanariadha nguli wa mbio fupi Usain Bolt amesema kuwa anatumai bado ataitimitza ndoto yake ya kuwa mchezaji kandanda wa kulipwa wakati atakapofanyiwa majaribio katika klabu ya Borussia Dortmund

https://p.dw.com/p/2qWRh
Leichtathletik WM London 2017- Usain Bolt
Picha: Reuters/M. Childs

Hata hivyo, bingwa huyo wa Olimpiki na dunia alikiri kuwa anapendelea kuichezea timu anayoipenda zaidi ya Manchester United.

Bolt mwenye umri wa miaka 31 ameliambia gazeti la Sunday Express kuwa atafanya majaribio mwezi Machi katika klabu ya BVB kabla ya kuamua kama ataweza kucheza kandanda. Mjamaica huyo anasema kama watasema yuko sawa, na kwamba anahitaji kufanya mazoezi, atafanya hivyo. Lakini kwa sasa ana hofu kwa sababu kandanda ni kitu tofauti na riadha na itabidi achukua muda ili kuzoea.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman