1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bomu lililofichwa kwenye gari la wagonjwa laua 95 Kabul

Iddi Ssessanga
27 Januari 2018

Wapiganaji wa kundi la Taliban wameripua bomu lililofichwa ndani ya gari la wagonjwa katika eneo lenye watu wengi mjini Kabul siku ya Jumamosi, na kuuwa watu wasiopungua 95 na wengine 158 wamejeruhiwa.

https://p.dw.com/p/2rd0x
Afghanistan Explosion in Kabul
Picha hii iliopigwa Jan. 27,2018 inaonyesha eneo la mripuko karibu na uwanja wa Sidarat mjini Kabul, Afghanistan.Picha: picture-alliance/dpa/Zumapress

Gari la wagonjwa lililokuwa limejazwa viripuzi limeripuka katika eneo lililojaa watu katika mji mkuu wa Kabul siku ya Jumamosi, na kuuwa watu wasiopungua 95 and kujeruhi wengine 158, maafisa walisema, katika mmoja ya miripuko zaidi kuutik,isa mji huo ulioharibiwa kwa vita katika miaka ya karibuni.

Mashambulizi hayo ambayo kundi la Taliban limedai kuyatekeleza -- ya pili kufanywa na kundi hilo katika mji mkuu wa Afghanistan katika kipindi cha wiki moja -- yamesababisha taharuki wakati manusurua waliojaw ana hofu wakikimbia eneo hilo lililotapakaa sehemu za miili ya binadamu, na hospitali zikizidiwa na idadi kubwa ya majeruhi.

Yamekuja wakati makundi yote ya Talibani na Dola la Kiislamu yakiimarisha mashambulizi yao dhidi ya Kabul, mmoja ya maeneo hatari zaidi kwa raia nchini Afghanistan.

Ripota wa shirika la habari la Ufaransa AFP, alisema aliona maiti nyingi na majeruhi katika hospitali ya Jamuriate, ambayo iko mita chache kutoka ulipotokea mripuko huo, na ambako wafanyakazi wa hospitali walikuwa wakipambana kuwatibu watu waliojaa damu wakiwa wamelala sakafu katika shoroba.

Taliban Anschlag in Kabul
Baadhi ya majeruhi wakiondolewa na kupelekwa kwenye usalama, kufuatia shambulizi hilo.Picha: picture-alliance/dpa/M. Hossaini

Vifo huenda vikaongezeka zaidi

"Idadi ya karibuni ya vifo imefikia 95 na majeruhi 158," Baryalai Hilali, mkurugenzi wa kituo cha habari cha serikali aliwaambia waandishi habari. Alionya kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka kutokana na ukweli kwamba wengi wa majeruhi waliopelekwa hospitalini hapo walikuwa katika" hali mbaya."

Mripuko huo ulitokea katika eneo ambako mashirika mengi makubwa, ukiwemo Umoja wa Ulaya, yana ofisi zake. Wanachama wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya mjini Kabul walikuwa katika "chumba chao salama" na hakukuwa na maafa yoyote kwa upande wao, afisa mmoja aliliambia shirika la AFP.

Mripuaji alipita angalau katika kituo kimoja cha ukaguzi akiwa katika gari la wagonjwa, akisema alikuwa anampeleka mgonjwa katika hospitali ya Jamuriate, alisema msemaji wa wizara ya mambo ya ndani. "Kwenye kituo cha pili cha ukaguzi, alitambuliwa na kuripua gari lake," alisema Nasrati Rahimi.

Dakika 20 kabla ya mripuko huo, ripota wa AFP aliona askari polisi wakikagua magari ya wagonjwa yakiwa mamia ya mita kutoka eneo la mripuko, huku madereva na wagongwa wakisimama mtaani. Magari ya wagonjwa hukaguliwa kwa nadra mjini humo.

Rais Ghani asema ni uhalifu dhidi ya ubinadamu

Anschlag in Kabul Afghanistan
Moshi ukitanda angani baada ya mripuko wa bomu mjini Kabul, Afghanistan, Januari 27, 2018, katika picha hii iliotoka kwenye mitandao ya kijamii.Picha: Reuters

Kundi la Taliban lilitumia mtadao wa kijamii kujitwika dhamana ya mripuko huo, ambao umetokea wiki moja kamili baada ya waasi wake kuivamia hoteli ya Intercontinental mjini Kabul, na kuuwa watu 25, wengi wao wakiwa raia wa kigeni.

Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zilizodaiwa kuwa na shambulizi hilo, ambalo rais wa Afghanistan alililaani haraka na kuliita "uhalifu dhidi ya ubindamu", zilionyesha moshi mkubwa ukifuka angani.

Karibu na eneo la mripuko, raia walikuwa wakitembea kupita katika vifusi vilivyofunika mitaa huku wakiwabeba majeruhi migongoni mwao, waketi wengine wakipakia maiti kadhaa kwa wakati mmoja kwenye magari ya wagonjwa na magari binafsi kuwapeleka kwenye vituo vya afya.

Tahadhari ya kiusalama iliotolewa Jumamosi asubuhi ilikuwa imeonya kuwa kundi la Dola la Kiislamu lilikuw alinapanga kufanya mashambulizi makubwa kwenye maduka makubwa ya kujihudumia (supermarket), maduka ya kawaida na hoteli zinazotembelewa zaidi na wageni.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/afpe

Mhariri: Zainab Aziz