1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bondia Pacquiao aomba radhi

17 Februari 2016

Bondia Manny Pacquiao amelazimika kuomba radhi kutokana na shutuma nyingi alizopata kutoka kwa wanaounga mkono mahusiano ya jinsia moja

https://p.dw.com/p/1HwWw
Manny Pacquiao besucht Todekandidatin Mary Jane
Picha: Getty Images/U. Ifansasti

Pacquaio ambaye pia ni mbunge nchini mwake Ufilipino alinukuliwa akisema kupitia televisheni kuwa vitendo vya ngono ya jinsia moja ni vibaya kuliko hata wanyama. Matamshi hayo yalizusha hisia kubwa kote ulimwenguni.

Bondia huyo alisema, kwa akili ya kawaida hata wanyama wanajua huyu dume huyu jike, mnyama dume hampandi mnyama dume na jike hampandi mnyama jike, kwa hivyo wanadamu tukiruhusu uhusiano wa jinsia moja basi tunafanya matendo mabaya kuliko hata wanyama.

Watu walipomzonga sana, akaweka mtandaoni, picha yake akiwa na mkewe, sasa wamemzonga zaidi kawaomba msamaha lakini akawaambia nimeusema ukweli kama ulivyo kwenye bililia, Mungu awabariki na ninawaombea.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Daniel Gakuba