1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bongo afariki.

Abdu Said Mtullya9 Juni 2009

Rais Omar Bongo wa Gabon amefariki.

https://p.dw.com/p/I5wh
Rais Omar Bongo wa Gabon afariki.Picha: picture-alliance/dpa

BARECELONA:
Rais Omar Bongo wa Gabon amefariki.

Habari juu ya kifo cha rais huyo zimethibitishwa rasmi na waziri mkuu Jean Ndong.Rais huyo alifariki jana kwenye hospitali ya mjini Bercelona nchini Uhispania, kutokana na maradhi ya moyo.Alikuwa na umri wa miaka 73.Rais Bongo aliitawala nchi yake kwa muda wa miaka 42.

Mtoto wake Ali Bongo ambae pia ni waziri wa ulinzi ametoa mwito juu ya kudumisha utulivu nchini kufuatia kifo cha baba yake.

Pana wasiwasi juu ya kutokea mvutano katika mchakato wa kumtafuta kiongozi mpya.Habari zinasema katika siku za hivi karibuni wanasiasa nchini Gabon wamekuwa wanachezeana turufu katika juhudi za kumtafuta mrithi wa rais Bongo.