1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Borussia Dortmund iko Zenit St.Petersburg

25 Februari 2014

Michuano ya kuwania ubingwa wa Ulaya, Champions League , inaendelea leo jioni kwa pambano kati ya Zenit St. Petersburg ya Urusi ikichuana na Borussia Dortmund ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/1BFCL
Fußball Champions League Achtelfinale Borussia Dortmund vs. Zenit St. Petersburg
Borussia Dortmund wakijipasha moto misuliPicha: picture-alliance/dpa

Sambamba na pambano hilo pia Manchester United iko ugenini ikiumana na Olympiakos Piraeus ya Ugiriki.

Fußball Bundesliga Borussia Dortmund gegen Eintracht Frankfurt
Aubamiyang wa DortmundPicha: picture-alliance/dpa

Hata hivyo Borussia Dortmund ambayo ni moja kati ya timu nne za Ujerumani zilizofikia awamu hii ya timu 16 bora barani Ulaya, inaandamwa na mkosi wa majeruhi, ambapo , kocha Jürgen Klopp amesema hana hakika iwapo mshambuliaji wa kikosi hicho Robert Lewandowski atateremka dimbani, baada ya kuugua homa ya mafua. Pia kikosi hicho kitakosa huduma ya mlinzi wake Mats Hummels pamoja na mchezaji wa kati Even Bender.

Wayne Rooney
Wayne RooneyPicha: picture alliance / empics

Kesho Jumatano Schalke 04 inaikaribisha nyumbani Real Madrid na kikosi cha kocha Jose Mourinho cha Chelsea kitapimana nguvu na Galatasaray ya Uturuki.